Aidha alisema kuwa, Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee.
Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kuwa, tishio la Korea Kaskazini ni kushambulia majirani zake kwa zana za nuklia.
Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan.
Tillerson amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo.
“Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu ya mabavu, na huu ni mpango hatari.”
“Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali,” Tisho la Korea Kaskazini la kufanya shambulizi la nuklia dhidi ya Korea Kusini au Japan ni la kuwezekana, na ni muda tu kabla ya Korea Kaskazini kufanikiwa kupata uwezo wa kushambulia Marekani.” alisema Tillerson.
0 maoni:
Post a Comment