Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
amewataka watanzania kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi ili waweze kubaini wahusika wa matukio ya uhalifu yanayotokea
nchini ikiwemo utekaji na kutoweka kwa baadhi ya watu akiwemo Ben
Sanane.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Akijibu
swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe
katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu bungeni Mjini Dodoma, amesema
watanzania wanapaswa kuwa watulivu na kuviamini vyombo vya uchunguzi
ambavyo vitakuja na majibu yatakayoonesha nini kinachoendelea nyuma ya
matukio hayo.
Mh. Mbowe alitaka kauli ya serikali
kuhusu matukio hayo, ikiwemo kutoweka kwa msaidizi wake Ben Sanane
ambaye hadi sasa ni takriban miezi mitano imepita tangu kijana huyo
atoweke, lakini akihoji sababu za serikali kutohusisha mataifa mengine
yaliyoendelea katika masuala ya kiuchunguzi hususani Uingereza katika
kufanya uchunguzi wa masuala ya aina hiyo.
"Kwanza nataka
nikuhakikishie kwamba Taifa letu lina mahusiano na mataifa kadhaa
ambayo tunashirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya ulinzi
... Taifa letu lina uwezo wa ndani wa kufanya ufuatiliaji wa kutambua
matukio haya ya awali, ya mtu kufariki ama kutoweka mahali baada ya
familia husika kutoa taarifa, tunaweza kufanya uchunguzi na kubaini
vyanzo, serikali haina kikomo cha uchunguzi kwa kutegemea na nature ya
tatizo lenyewe, uchunguzi huu utakapokamilika, taarifa itatolewa" Alisema Majaliwa
Waziri mkuu amesema “Tukitoa taarifa mapema tunaweza
kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia
kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini
chanzo chake alisisitiza,”.Kadhalika Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.
Kwa upande mwingine, Majaliwa amemjibu
Kiongozi wa Upinzani kuwa suala la kurusha matangazo mubashara ya
shughuli za Bunge yalishafikiwa katika Bunge lililopita na serikali
itaendelea kuboresha kila
wakati namna ya urushwaji wa matangazo hayo.
0 maoni:
Post a Comment