Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU
pamoja na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda
kukusanya mapato pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanaodaiwa
sugu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Akijibu
swali la Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi
cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa
kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa kuwa wapo baadhi ya
wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa madeni na
badala yake hutoa rushwa.
Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya
serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na
kuwatisha wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa
inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na
TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza , Arusha na
Mbeya.
“Ni kweli kwamba tunacho
chombo ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi
kutoka kwa walipa kodi wetu wafanyabiashara wakiwemo, lakini TRA kutumia
‘task force’ haina maana ya kuwatishia amani wafanyabiashara ila lengo
lake ni kufuatilia wadaiwa sugu japokuwa siyo wote ila wachache hawataki
kabisa kulipa pamoja na kwamba wanajua wao ni wadaiwa sugu.....
Tunatumia TAKUKURU kwa sababu kuna wengine hutumia fursa hiyo kutaka
kuwahonga maafisa wa TRA ili wafutiwe madeni yao”. Alisema Majaliwa
Vile vile Majaliwa amesema ‘task force’
imeundwa na TRA wenyewe ili kuona wanapokwenda kukusanya madeni yao
hakutumiki vitendo ambavyo havikubariki kama vile utoaji wa rushwa ili
madeni hayo yasilipwe au namna nyingine yoyote ambayo mfanyabiashara
anaweza kuona si sahihi kwake.
0 maoni:
Post a Comment