Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol, amesema kuwa Baba yake mzazi alifungwa kifungo cha miaka miwili wakati mama yake mzazi akiwa na ujauzito wake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘ Phone’, amesema baaada ya kuzaliwa alipelekwa na Mama yake gerezani na Baba yake kumpatia jina la ‘Majuto’.
“Baada ya 40, Mama akanipeleka gerezani akaniweka mimi pale kwenye dirisha la kuongea na wafungwa ndipo nikapewa jina pale, sijawahi kusema popote nikaitwa ‘Majuto’. Lakini baada ya kuja kubatizwa ndio nikaitwa Bernard,” Ben Pol alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM.
Pia alisema wakati baba yake yupo gerezani, Mama yake alimlea kwa biashara ya vitumbua pamoja na kuuza maji.
Ben amesema baada ya miaka miwili, Baba yake aliachiwa na kuendeleza gurudumu la maisha kama kawaida.
0 maoni:
Post a Comment