Msanii wa muziki Tanzania, Linah Sanga, ameelezea sababa za ukimya wake kusababishwa na kutokuwepo sawa kiafya.
Linah amesema hayo kupitia kipindi cha FNL cha EATV jana usiku ,”Nilikuwa naumwa kwa kweli na pia hii ni mara yangu ya kwanza kuwa katika hali hii (Ujauzito) so nikawa naumwa ndio maana nilikuwa kimya kwa muda. Wakati ninagundua nipo hivi mimi na muhusika tuligombana ila hatukuachana ,baada ya kufanya vipimo, nakuhakiki hali ya ujauzito wangu, nilimtext mhusika na akafurahi sana na tupo mpaka leo.
Kwa sasa Linah sasa yupo chini ya record label ijulikanayo kama Dropouts Entertainment, inayomsimamia yeye pamoja na msanii aitwaye Mr. Kesho.
Kwa sasa Linah anatamba na ngoma ya Mfupi ft G.Nako.
Na Laila Sued
0 maoni:
Post a Comment