Herrera mchezaji bora wa mwezi Man U




Klabu ya Manchester United imemteua kiungo Ander Herrera kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili ndani ya klabu hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo iliyopita.

Mspaniola huyo amepata asilimia 46 ya kura akimzidi Eric Bailly na Marcus Rashford ambao wote wamepata asilimia 27. Herrera alikabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa AON Complex baada ya kuisadia United kushinda 1-0 nchini kwao, Hispania dhidi ya wenyeji Celta Vigo kwenye nusu fainali ya kwanza ya Europa League.

Ander Herrera baada ya kukabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa Aon Complex
Hii inakuwa mara ya tatu kwa kiungo huyo kushinda tuzo hiyo, baada ya kushinda pia Februari na Aprili 2015.Herrera amekuwa katika kiwango kizuri siku za karibuni kwenye Ligi Kuu ya England na zaidi aling’ara kwenye mchezo dhidi ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Chelsea,The Blues.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment