Chelsea yabakiza michezo miwili kuwa Bingwa







Wapinzani wa klabu ya Chelsea,Tottenham Hotspur imekubali kipigo cha goli 1 kwa 0 mbele ya wagonga nyundo wa landani klabu ya West Ham United katika mchezo uliopigwa hapo jana wa ligi kuu nchini Uingereza.
during the Premier League match between West Ham United and Tottenham Hotspur at the London Stadium on May 5, 2017 in Stratford, England.
Spurs ndio klabu pekee inayomkimbiza kiongozi wa ligi, The Blues, katika mbio za kuwania Ubingwa na kwa matokeo hayo sasa klabu ya Meneja Antonio Conte, Chelsea ina njia nyeupe ya kutwaa taji la ligi kwa msimu huu endapo itafanikiwa kushinda michezo miwili ya ligi.
Alie kuwa Mwiba mchungu katika mchezo huo wa Spurs dhidi ya West ham ni mchezaji Manuel Lanzini alietokomeza ndoto za spurs kutwaa ubingwa msimu huu mara baada ya kupachika bao lake dakika ya 65 lililotosha kabisa kuilaza klabu hiyo.

Klabu ya Chelsea, mpaka sasa wanaongoza katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa kuwa na alama zao 81 katika michezo 34 iliyo cheza, ilhali klabu ya Spurs ikishika nafasi ya pili wakiwa wamejikusanyia alama 77 kibindoni huku wakiwa wameshuka dimbani mara 35.
BY HAMZA FUMO
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment