Rapa Jay Moe anasema kama
akipata nafasi ya kukutana na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe
Magufuli hataweza kumshauri jambo lolote kwa kuwa yule ni Rais wa nchi
bali yeye atamuomba awafikirie wasanii na kuona umuhimu wao.
Jay
Moe amesema hayo na kusisitiza wasanii walikuwa na mchango mkubwa
katika uchaguzi uliopita ambao umesaidia viongozi wengi kuingia
madarakani
"Nitamuomba Magufuli maana
siwezi kumshauri yule ni Mh. Rais wa nchi bali nitamuomba atufikirie na
aone umuhimu wetu, kwa sababu mchango wetu umetumika sana katika
uchaguzi uliopita, tumeweza kwenda 'endorse' kuithinisha wagombea na
vitu kama hivyo kwa hiyo waone kwamba imefika muda na wao kutoa shukrani
kwa kile ambacho sisi tulikifanya kwa kufanikiwa kwao kushinda,
matatizo yetu sisi wasanii yanajulikana tuna mfumo mbovu sana wa masoko,
mzuki wetu mzuri lakini haujulikani utauzwa wapi nadhani kupitia
serikali na idara zake kama COSOTA, BASATA, Waziri wanaweza wakakomaa
wakaweka nguvu fulani" alisema Jay Moe
0 maoni:
Post a Comment