Mkongwe aliyerudi kwenye game
kwa kasi nzuri, Juma Mchopanga 'Jay Moe' amefunguka na kusema kwamba
kwenye nyimbo zake alizoweza kuandika na ku-diss watumiaji wa unga
ilikuwa ni njia ya kufikisha ujumbe kwa marafiki zake na wasanii kwa
njia ya sanaa.
Mwanamuziki Juma Mchopanga 'Jay Moe'
Jay
Moe ameweka wazi hayo baada ya kuulizwa juu ya mstari wake ' bora mimi
sikuwa na zali maana waliopata zali sasa hivi ni mateja hatari" kuwa ni
kweli aliandika kwa ajili kuwadiss wasanii wenzake waliokuwa wanatumia
madawa ya kulevya.
Jay Moe amesema kuwa kwa muda mwingi
amekuwa balozi wa kukemea matumizi ya dawa za kulevya kwa wasanii kwani
imekuwa ikileta picha mbaya kwa wazazi ambao wataanza kuwaza kama
mwanaye akiwa msanii basi baadae akipata umaarufu lazima atajidumbukiza
hwenye dawa za kulevya.
"Mimi nmezaliwa katika
mazingira ya dini na yanayofundisha kutokukata tamaa. Sasa wasanii
wanaotumia vigezo vya game ngumu ndio maana wanaingia kwenye madawa ni
uongo, kwa sababu kutumia madawa ni kukata tamaa ya kuhangaika kama
kijana . Lakini kama unaweza ukaaingia kwenye madawa ukawa unatumia hata
laki kwa kusema unamaliza stress ugumu wa game unakuja vipi hapo.
Tatizo wengi wao wanashindwa ku-confess kama kuiga iga ndo kumewaponza.
Mwisho wa siku wanakuja kutuchoresha sisi wengine ambao tunapambana
kuwaaminisha wazazi huu muziki siyo uhuni.
Mwanamuziki Jay Moe
"Aidha Jay ameongeza kuwa "Nilitumia
wimbo kuwachana hadi washkaji zangu kwa sababu najua ingewatia hasira
kuliko ningemwambia tukiwa wawili, ningemuambia kishkaji lakini kwenye
ngoma inasikilizwa na mamilioni ya watu hivyo mtu anajishtukia na wapo
watu wengi walikuja ku confess wameacha na wengine wamehitaji ushauri. Jay Moe aliongeza.
0 maoni:
Post a Comment