Msanii kutoka 'Green City'
akiwakilisha kundi la The Amaizing, Izzo Bizness amedai hawezi kulala
njaa kusubiri simu za promota kwa ajili ya show kwani kipaji anacho ndio
maana anajiongeza zaidi mikoani.
Msanii Izzo Bizness
Izzo
amefunguka hayo baada ya maswali mengi kuzuka kwa nini hana 'show'
nyingi Dar Es salaam kama mikoani, na kueleza kwamba muziki ni biashara
yake hivyo hataweza kubweteka huku biashara yake inaharibika..
"Sikai kutegemea mpaka
Promota anipigie simu kuhusu show maana hapo kuna kuna kuanza mazungumzo
na kushushana bei, ila natengeneza mwenyewe najijua mikoa flani ndani
ya Tanzania nakubalika nachukua opportunity hiyo kutengeneza show hizo
peke yangu na mwisho wa siku maisha yanaendelea. Haipendezi msanii kama
mimi nianze kupiga vizinga hadi vya vocha , Hata prof. Jay aliwahi
kusema kama kipaji unacho kwa nini ufe na njaa, na ndivyo nifanyavyo
mimi ", Izzo alifafanua
Aidha Izzo ameongeza kwamba pamoja na
changamoto kama kundi la The Amaizing wanazokumbana nazo amewataka
wasanii waimbaji wajipange sana kwani ujio wa Abella Music lazima
uwatingishe kwenye game.
"Kwa sasa The Amaizing tuna
changamoto ukizingatia Abella ni mgeni ndo anaanza kutengeneza mashabiki
kwa hiyo na uhakika akishapata kile anachohitaji atakuwa moto balaa na
nitoe angalizo kwa waimbaji siyo kwa kuwa-disrespect hapana ila ujio wa
Abella lazima uwasumbue hivyo wajipnge sana", Izzo aliongeza.
0 maoni:
Post a Comment