Sadiki aliliambia gazeti la Habarileo, kuwa Rais hajakosea kumteua Mghwira kuwa kiongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwani mwana mama huyo ni mchapakazi, mzalendo na asiye na ubaguzi, na uongozi unahitaji mtu wa aina hiyo.
Meck alisema kuna maeneo matano ambayo angependa mteuliwa huyo ayape kipaumbele ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji. Alisema kama mazingira yataharibiwa zaidi ndani ya miaka 10 mkoa utakuwa jangwa na kukumbwa na baa la njaa. Katika eneo hilo, alitaka Mghwira ashirikiane na taasisi na viongozi wengine kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Hata hivyo eneo jingine alisema ni uvushwaji wa bidhaa za magendo kutoka Tanzania kwenda Kenya. Alisema mkoa unakosa mapato mengi kutokana na mbinu za ujanja za wafanyabiashara wasio waaminifu. Alimtaka kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kujipanga vyema kudhibiti hilo. Dawa za kulevya Alisema kuwa zimekuwa zikiathiri maendeleo ya mkoa.
Bi Anna anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadiki.
0 maoni:
Post a Comment