Waziri Mkuu aahidi kutuma mkaguzi Gairo





 
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aahidi kutuma mkaguzi kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo, mkoani Morogoro.

Waziri Majaliwa ametoa ahadi hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Gairo ‘A’.
Waziri Majaliwa alisema “Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu, ili tupate picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje. Huyu mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zake.”
“Kwenye mkutano wangu na watumishi wa Serikali nimewaeleza kwamba ninyi ni desk officers (maafisa wa kukaa ofisini tu), wala hamuendi vijijini kuona hali halisi ikoje. Ndiyo maana wananchi hawa wanalalamikia kukosa dawa na wewe wala hujui,” alisema.
“Ni lazima uende kwenye vituo vya afya na zahanati na ucheki matumizi ya dawa la sivyo unaweza kupata kesi kama ya Shinyanga ambapo mganga wa kituo cha afya alikutwa na dawa za Serikali nyumbani kwake, baada ya wanachi kumwekea mtego hadi akakamatwa.”
Aidha Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kumhoji Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Albert Lyaruu kama anamiliki duka la dawa au la na kujibiwa kwamba hana duka la dawa. Lakini pia Dk. Lyaruu alikiri kwamba baadhi ya watumishi wa idara yake wanayo maduka ya dawa.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment