Qatar
Mataifa sita ya Kiarabu
yakiongozwa na Saudi Arabia na Misri, yamesitisha ushirikiano wa
kidiplomasia na nchi ya Qatar kwa madai kuwa inaunga mkono makundi ya
kigaidi.
Qatar imeshtumiwa kuunga mkono
makundi kama Islamic State na al-Qaeda, ambayo yanaendelea kuwa tishio
kwa usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.
Mataifa mengine yaliyotangaza hatua hiyo ni pamoja na Bahrain, Falme za Kiarabu, Yemen na Libya.
Qatar imekanusha madai hayo na kusema, hakuna ushahidi wowote kuonesha kuwa inashirikiana na makundi hayo na inahatarisha usalama Mashariki ya Kati.
Mataifa hayo ya kiarabu yamesema yamechukua hatua hiyo kwa maslahi yao ya kitaifa pamoja na maswala ya kiusalama.
Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Bahrain zimewataka raia wa Qatar kuondoka nchini humo ndani ya wiki mbili.
Uturuki imesema iko tayari kuongoza mazungumzo kati ya Qatar na Mataifa hayo ya kiarabu.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kilichotokea kati ya nchi hizo za kiarabu na Qatar.

0 maoni:
Post a Comment