Tiketi za michuano ya SportPesa Super Cup zaanza kuuzwa


Michezo

 



Kuelekea michuano ya kombe la SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza kesho Juni 05, 2017, tayari tiketi zimeanza kuuzwa rasmi kupitia Kampuni ya Selcom, ambapo bei za tiketi za VIP ni 15,000/- na 10,000/- wakati bei za tiketi za kawaida ni 3,000/- tu.

Wadau wa mpira wenye kadi za Selcom wameanza kupata kadi za mechi hizo na wengine wanaweza kununua tiketi za mechi husika kuanzia saa tatu kamili asubuhi uwanja wa Uhuru.  SportPesa na Selcom inawatangazia wapenzi wa soka kununua kadi za Selcom kwa muuzaji aliyepo karibu yao.
Michuno ya SportPesa Super Cup itafanyika katika uwanja wa Uhuru uliopo pembezoni mwa Uwanja wa Taifa, ambapo itazikutanisha timu 4 kutoka Tanzania na timu 4 kutoka Kenya katika kuwania kitita cha Dola za kimarekani elfu thelathini (US $ 30,000) sawa na Tsh milioni 62 na mshindi wa fainali hizo atapata nafasi ya kuvaana na timu ya Everton kutoka Ligi kuu ya England mwezi Julai 13 mwaka huu.
Wapenzi wa soka wanaweza kununua tiketi za mechi kupitia simu zao za mkononi kwa kufuata hatua zifuatazo:
1. Kwa wateja wenye kadi za Selcom bonyeza *150*50#, kisha andika namba ya kadi yako ya Selcom, kisha chagua namba 3 ambayo ni burudani /Michezo.
2. Weka pesa kwenye kadi kupitia wakala au duka la Selcom, au kupitia kadi nyingine ya Selcom.
3. Wateja wanaotumia mtandao wa Airtel wanaweza kuweka pesa kwenye kadi zao kupitia Airtel Money kwenda namba ya biashara 172255.
4. Kwa wateja wanaotumia huduma za benki kwa njia ya simu (Mobile Banking) wanaweza kuweka pesa kwenye kadi zao za Selcom kupitia Akiba Commercial bank, Exim Bank, Mkombozi Bank na Stanbic Bank au kwa kutembelea tawi lolote la Akiba Bank na NMB Bank na kujaza kadi moja kwa moja.
Ratiba ya michuano ya kombe la SportPesa Super Cup
Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza kwa AFC Leopards ya Kenya kuchuana na Singida United huku mabingwa wa Vodacom Premier League Yanga SC wakichuana na mabingwa wa SportPesa Premier League Tusker FC ya Kenya siku ya tarehe 6.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment