Kocha Zinedine Zidane huwenda akaifundisha klabu ya Real Madrid maisha yake yote kwa mujibu wa rais wa klabu hio, Florentino Perez ikiwa ni siku chache baada ya kocha huyo Mfaransa kuchukua kombe la Champions League kwa miaka miwili mfululizo, baada ya ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Juventus.
Meneja huyo ambaye pia alikuwa na mafanikio makubwa katika kucheza soka duniani, alikuwa akibezwa hukusu uwezo wake wa kufundisha soka.
Ubingwa huo umeweza kuifanya klabu hiyo kuvunja rekodi ya kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo pamoja na kuwa klabu iliyochukua kombe hilo mara 12.
Rais wa klabu ya Real Madrid ameiambia radio ya Spanish Cadena Ser “Zidane can stay at Real Madrid for the rest of his life. Every Real Madrid fan is so grateful to him, he lifted our level of talent when he arrived in 2001 and was the best player in the world,”
Kwa upande wa Zidane baada ya mafanikio hayo alisema, “I can’t say whether I’ll stay for the rest of my life but I’m so grateful for the club for everything it has given me,”
“I played here for a long time and I feel part of the furniture. I’m also lucky to be part of this club and with this squad. Every player in the squad has played their part, and that’s been the key factor this season.” Zidane aliviambia vyombo vya habari.
0 maoni:
Post a Comment