Polisi wakiwa wamesimama mbele ya gari ambalo lilitumika kuwagonga waenda kwa miguu mjini Melbourne, Australia. 21 Desemba
Gari
limewagonga waenda kwa miguu kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini
Australia, Melbourne, katika tukio ambalo polisi wanasema lilikuwa la
kukusudiwa ambapo watu zaidi ya 14 wamejeruhiwa kati yao wakiwa na
majeraha mabaya.
Kwa
mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa watu walionekana
kurushwa juu wakati gari hilo lilipokuwa likiwagonga waenda kwa miguu na
hakukuwa na dalili za dereva kusimama.
Idara ya
polisi kwenye kituo cha Victoria wamesema kuwa wanawashikiliwa watu
wawili akiwemo dereva wa gari ambaye aliwagonga waenda kwa miguu jirani
na kituo cha basi chenye watu wengi mjini Melbourne.
Polisi
wanasema kuwa “tunaamini kutokana na kile tulichokiona, kuwa tukio
lilifanywa kwa makusudi. Lakini hatujui bado chanzo chake,” alisema
kamanda wa kituo cha Victoria Russel Barrett.
Hata
Barrett hakuweza kugusia ikiwa tukio hili lina uhusiano wowote na
ugaidi ingawa amekiri uchunguzi wa awali umaeanza kufanywa.
Vikosi vya uokoaji vimesema viliwachukua watu kadhaa kuwapeleka Hospitali kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Polisi wametoa wito kwa raia kuchapisha picha zozote ambazo wanaweza kuwa walirekodi wakati wa tukio.
0 maoni:
Post a Comment