Siasa - Uchumi
Wananchi wa Uingereza kuwachagua wabunge 650 kwa minajili ya kuundwa kwa serikali mpya
Mamilioni ya wananchi wa Uingereza wanapiga kura kuwachagua wabunge wapya, huku chama kitakachoshinda kikiunda serikali.
Kuelekea
kwenye Uchaguzi huu, vyombo vya Habari nchini humo vinabashiri kuwa
Chama cha Waziri Mkuu Theresa May cha Conservative, kinaongoza kwa
asilimia 41.5 huku kile cha Labour ikiwa na aslimia 40.4, kwa mujibu wa
vyombo vya Habari nchini humo.
Ushindani mkubwa ni kati ya viongozi wa vyama hivyo viwili, Waziri Mkuu Theresa May na kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn.
Ni uchaguzi unaokuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na hatari ya kushambuliwa na magaidi lakini baada ya kuanza mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.
Chama kitakachoshinda idadi kubwa ya viti bungeni kati ya 650 vinavyowaniwa, ndicho kitakachounda serikali.
Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa mchana.

0 maoni:
Post a Comment