Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati akijibu maswalia ya wabunge mjini Cap, Mei 31, 2017
Uchumi
wa Afrika Kusini umeyumba zaidi kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha
miaka minane. Upinzani unamtaka rais Jacob Zuma ajiuzulu ukimshtumu kuwa
yeye ndio anasababisha hali hiyo.
Kati
ya mwezi Januari na Machi mwaka huu, uchumi wa taifa hilo ambalo zamani
lilikuwa liongoza barani Afika kwa uchumi, uchumi wake umeshuka kwa
asilimia 0.7.Thamani ya sarafu ya Euro nayo imeshuka kwa asilimia 1.
Upinzani nchini humo wameendelea kushutumu uongozi wa rais Jacob Zuma ambaye wanamtuhumu ni mfisadi kuchangia pakibwa katika hali hii, madai ambayo hata hivyo rais Zuma ameyakanusha.
Zuma anaendelea kukabiliwa na tuhuma za rushwa na ufisadi, huku nchi yake ikiendelea kukumbwa na maandamano ya hapa na pale.
0 maoni:
Post a Comment