Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuambia Spika wa bunge, Job Ndugai kuwa baadhi ya wabunge ambao wanaoropoka bungeni anaenda nao vizuri huku akisema anawasubiri waropoke tena nje ya bunge ili adili nao vizuri.
Rais Magufuli aliyasema hayo wakati akipokea ripoti ya pili iliyounda kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa madini kwenye makontena ya mchanga, Ikulu jijini Dar e salaam jana.
“Spika Job Ndugai nitakuletea mizigo hii bungeni, lakini kwa wale wanaoropoka bungeni naona unaenda vizuri nenda na mwendo huo huo. Maana wakiwa kule wanaweza kutukana wanalindwa na kinga ya bunge, ila ukiwatimua mwezi mzima wataropoka nje ya bunge, mimi nitadili nao vizuri,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa
“Siwatishi bali nawaambia ukweli huwezi kuwa unarudisha watu nyuma kwenye vita hii, kama huna la kusema ni bora ukae kimya.”
0 maoni:
Post a Comment