millardayo.com na Ayo TV zimempata Kamanda wa Polisi Mwanza Ahmed Msangi ambaye kwanza alithibitisha kutokea ajali hiyo lakini akasema pia walikuta silaha pamoja na kiasi kikubwa fedha kimeteketea.
Kamanda Msangi amesema>>>“Mzee anaitwa Maduhu Masunga Ligushi ama kwa jina maarufu sana anaitwa Mzee Shinyanga…alifariki dunia kutokana na ajali ya moto ambao uliunguza nyumba yake kisha kujeruhi watoto wake wawili.”
Aidha, Kamanda Msangi amesema kuwa mbali na kusababisha kifo na kujeruhi moto huo pia umeunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilikuwa ndani pamoja na silaha.
“…na kusababisha vile vile uharibifu wa vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo ikiwemo kiasi kikubwa cha pesa ambacho mpaka sasa hivi bado hatujafahamu kilikuwa kiasi gani lakini kilikuwa kiasi kikubwa sana lakini pamoja na silaha mbili; bastola revolver na Short Gun.”
Kamanda Msangi ameelezea pia ajali hiyo akisema: “Inasemekana kwamba kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu alikuwa ndani pamoja na watoto wake lakini ghafla ukazuka moto mkali ambao ulikuwa unaunguza nyumba hiyo. Inadaiwa kuwa kutokana na hali hiyo marehemu hakutaka kuondoka kwa haraka kwa sababu kulikuwa na vitu vyake alikuwa anataka kuvitoa. Inawezekana ni pesa au vitu vya thamani ama vitu vingine vya thamani ambavyo yeye anajua alikoviweka lakini wengine walikuwa wameanza kukimbia kujiokoa kutoka kwenye ile nyumba.” – Kamanda Msangi.
0 maoni:
Post a Comment