Kama uko katika umri huu uko katika hatari ya kupata kansa ya utumbo mpana!

Image may contain: food
Utafiti uliochapishwa katika jarida moja la kansa huko Marekani umebainisha kuwa hatari ya kupata ugonjwa wa saratani imeongeza miongoni mwa watu wenye umri kati ya miaka 20-39 na 40 - 54. Hata hivyo kundi la watu wenye umri kati ya miaka 20 - 39 wako katika hatari kubwa zaidi kuliko wale wenye miaka 40-54
Kufunga choo,kupata choo chenye damu pamoja na upungufu wa damu zinaweza kuwa dalili za saratani ya utumbo mpana.
Mambo ambayo huweza kuongeza uwezekano wa kupata kansa za namna hii ni uzito mkubwa (unene/kitambi) kutofanya mazoezi na aina za vyakula mfano matumizi makubwa ya nyama nyekundu (nyama ya ng'ombe,maini,nyama ya kondoo), na vyakula vilivyokaangwa katika joto la juu (chips)
Vyakula vya nafaka,matunda pamoja na mboga za majani hupunguza hatari ya kupata kansa ya utumbo mpana.
Sababu zingine ambazo huweza kuzuilika ni pamoja na uvutaji wa sigara na bidhaa za tumbaku na pombe.
Sababu ambazo haziwezi kuzuilika ni pamoja na umri,historia ya magonjwa ya namna hii katika familia na maradhi mengine.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment