Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ikicheza na Zambia mchezo wa Nusu Fainali ya CODAFA
Timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) imekuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Taifa Stars kwa jumla ya magoli 4-2 katika hatua ya Nusu Fainali mchezo ulichezwa katika dimba la Moruleng nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo huo beki wa Stars, Erasto Nyoni alianza kuipatia Taifa Stars bao la kuongoza katika dakika ya 14, lakini katika dakika ya 44 Brian Mwila, akaisawazishia goli hilo ’Chipolopolo’ dakika moja baadae Justin Shonga akaifungia Zambia goli la pili.
Wakati wa kipindi cha Pili, dakika ya 56 Chipolopolo wakaongeza goli la tatu kupita kwa Chirwa aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Justin Shonga akahitimisha karamu ya magoli wakati Simon Msuva akiishindia Stars gold la pili mchezo uliomalizika kwa idadi hiyo ya magoli na Zambia kutinga Fainali.
Wakati Zimbabwe imetinga hatua ya Fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya Lesotho kwa jumla ya magoli 4-3 kwa matokeo hayo inaifanya Zimbabwe kucheza na Zambia katika mchezo wa fainali utakao chezwa siku ya Jumapili ya Julai 9.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA Castle Cup utazikutanisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Lesotho siku ya Ijumaa.
Wachezaji wa Timu ya timu ya taifa ya Zambia na Zimbabwe
0 maoni:
Post a Comment