Bunge lavamiwa na wafuasi wa Maduro


mediaWafuasi wa serikali ya Venezuela wamshambulia mtu ndani ya eneo la Bunge mjini Caracas, 5 Julai 2017
 
Bunge la Venezuela linalodhibitiwa na upinzani, lilivamiwa Jumatano Julai 5 jioni, baada ya kuzingirwa kwa muda wa saa saba na waandamanaji wanaomuunga mkono rais Nicolas Maduro.
Wabunge wasiopungua watano na wafanyakazi saba wa bunge walijeruhiwa katika uvamizi huo. Rais Nicolas Maduro amekanusha kuhusika kwake katika vurugu hizo. Marekani imeshutumu hali hiyo ikibaini kwamba "uvamizi huo haukubaliki".
Bunge hilo lilivamiwa na wafuasi kadhaa wanaounga mkono serikali ya Nicolas Maduro wakati ambapo wabunge walikua katika kikao. Bunge hili lina wabunge wengi kutoka upinzani tangu uchaguzi wa wabunge wa mwezi Desemba 2015.
Wafuasi hao wa rais Maduro, baadhi walikua walijificha nyuso, huku wakibebelea marungu na walikua walivaa nguo nyekundu - rangi ya chama tawala. Watu hawa walirusha mawe na mabomu yaliotengenezwa kienyeji, na kusababisha hofu. Wakati huo makabiliano yalizuka. Wabunge wa upinzani walijeruhiwa. Mmoja aliepigwa kichwani, alipelekwa hospitalini na gari la wagonjwa.
Tukio hili la vurugu linakumbusha mvutano uliotokea wiki iliyopita wakati wabunge kadhaa walituhumu makundi ya vurugu kuwazuia kwa saa kadhaa kutoka katika jengo la Bunge. Wabunge na waandishi wa habari walitoka ndani ya jengo hilo kwa msaada wa polisi siku ya Jumatano jioni.
Rais Maduro aamuru kuanzishwa uchunguzi
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amekanusha kuhusika kwake katika vurugu hizo. "Ninalani uvamizi huo. sihusiki kabisa na vurugu hizo, "alisema, na kuthibitisha kuwa ameamuru uchunguzi ufanyike. Tukio hilo linakuja wakati ambapo Venezuela inaendelea kukumbwa na mgogoro wa kiuchumi na kisiasa, huku wimbi la maandamano likiendelea kushuhudiwa nchini humo, ambapo waandamanaji wanamtaka rais Nicolas Maduro ajiuzulu. Waandamanaji wanadai kwamba watu 91wameuawa na kikosi cha rais Maduro kwa muda wa miezi mitatu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment