Marekani kupitia balozi wake
katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, imesema kuwa itatumia nguvu za
kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini “iwapo itahitajika”. Kauli hiyo inakuja
siku mbili tu baad aya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora la
masafa marefu linalotoka bara moja kwenda hadi bara jingine.
Bi Haley alisema siku ya Jumatano
kwamba jaribio la kombora la masafa marefu la Korea Kaskazini ICBM
linaangamiza suluhu ya uwezekano wa mazungumzo ya kidiplomasia.
''Marekani imejiandaa kutumia uwezo wake wote kujilinda na washirika wetu'', Bi Haley aliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo lilikutana kwa kikao cha dharura kuzungumzia hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
Bi Haley ambaye alisema alijadili swala hilo na rais, alisema kuwa Marekani pia inaweza kukata biashara na mataifa ambayo yanaendelea kufanya biashara na Korea Kaskazini kwa kukiuka maamuzi ya Umoja wa Mataifa.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio hilo ambalo linakiuka marufuku ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, licha ya vitisho vya Marekani na Umoja wa Mataifa.
Hivi karibuni Marekani ilisema kuwa haitokubali Korea Kaskazini kuendelea kukiuka sheria kwa kufanya jaribio la makombora yanayokiuka marufu ya Umoja wa Mataifa.
Nikki Haley alisema kuwa maamuzi mapya pia yatawasilishwa dhidi ya Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, huku akilezea jaribio hilo kama tishio la kijeshi dhidi ya Marekani na dunia kwa ujumla. Baloi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ametishia kutumia vikwazo vya kibiashara.
Nae waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis na mwenzake wa Japan Tomomi Inada walisema kuwa jaribio hilo ni uchokozi ambao hautakubalika.

0 maoni:
Post a Comment