Kuna mtu ameniuliza je kauli ya Ronaldo kuwa amejitangaza mchezaji bora wa dunia muda wote naichukuliaje? Nimemjibu kirahisi sana. Ndio yupo sahihi. Ameniuliza kwanini? Nikamjibu kwa sababu Ronaldo amesema. Akaniuliza tena ina maana Lionel Messi, Ronaldinho Gaucho, Pele, na Diego Maradona wamezidiwa na Ronaldo? Najua lengo lao wanazungumzia kipaji. Nikamuuliza hao uliowataja wamemzidi nini Ronaldo. Wataniambia Ronaldinho ana chenga Messi ana balaa na Pele alifunga magoli pipa zima.
Walio wengi wanachanganya mambo. Sijui kwanini wanapapatika kwa kauli hii ya Ronaldo.
Ronaldo anaona ana mafanikio ambayo wengine hawana. Hakuna mchezaji aliyewazidi wachezaji wote duniani kila kitu. Soka ni kama choo kila mwenye divi anaingiamo, uwe unaendesha uwe una magogo au unaenda kukojoa wewe una haki ya kuingia. Ronaldo anafahamu alichomzidi nacho Pele, na anaona kipo ambacho maradona hawezi kujivunia. Yapo aliyozidiwa na wenzake na yeye ana rekodi zake ambazo hao mnawaona bora hawanusi. Kwanza ni mchezaji pekee duniani ambaye amefunga kila dakika. Ni mchezaji pekee aliyefunga magoli zaidi ya 50 kwa mwaka ndani ya miaka 6. Mchezaji wa kwanza na pekee aliyefikisha magoli 100 ya UEFA.
Msishushe Ronaldo kisa watu mliohadithiwa. Ndugu zangu kinyesi cha kale hakipimwi maradhi. Hebu tusing’ang’anie kiporo cha piza tena za juzi kisa hamtaki mihogo ya sasa. Ronaldo ni mchezaji bora duniani wala hupaswi kuongea taratibu. Kama nyie hamtaki kuthamini alichofanya kwanini asisifie mtarimbo wake? Mwanaume sifia mzizi wako ili watu wasichukue mti wako.
Kila aliye bora na asimamie ubora wake. Mwanaume mwenye uchu wa mafanikio hasifii mali za mwanaume mwingine ila hujigamba kwa kile alicho nacho. Hakuna kigezo cha nani ni bora hivyo kila mtu apambane na hali yake.
0 maoni:
Post a Comment