Rais wa Uganda aidhinisha sheria ya kuondoa kikomo cha umri wa rais


mediaYoweri Museveni, rais wa Uganda.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameidhinisha sheria inayoondoa kikomo cha umri wa rais nchini humo na hivyo kumruhusu kuwania katika uchaguzi wa urais mwaka 2021.
Sheria ya awali ilikuwa inamzuia mgombea kuwania urais baada ya kutimiza umri wa miaka 75. Kulingana na sheria hiyo ya awali Yoweri Museveni, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 73 hangeliweza kuwania katika uchaguzi ujao.
Bunge liliidhinishwa mswada huo mnamo tarehe 10 Desemba kwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge waliohudhuria kikao, wabunge 317 wakiunga mkono na 97 wakapinga.
Hatua ya rais Museveni kuidhinisha mswada huo imekuja wakati ambapo amekuwa akihimizwa na viongozi wa kidini na wanaharakati wa kisiasa kutouidhinisha.
Hata hivyo mswada huo unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.
Kama rais Museveni atashinda uchaguzi wa 2021 ataongoza nchi ya Uganda hadi 2031.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment