AJALI YAUA 1 MBEYA NA KUJERUHI 9 MBEYA.

jichopembuzi@gmail.com
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 9  kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gali iliyotokea jana saa 9:00 katika kijiji cha LUWATI barabara ya KAMSAMBA MLOWO wilayani MBOZI mkoani  MBEYA.

Habari toka kwa maafisa wa polisi zinasema kuwa gari lenye namba za usajili T855 ACJ aina ya  MISTUBISHI FUSO lililokuwa likiendeshwa na dereva CREMENT EXAVERY kupinduka kisha kusababisha kifo cha LAUDEN MWAMPANGALA 17  MKULIMA,MNYIA na mkazi wa NAMBINZO na kuwajeruhi wengine 9 ambao wamelazwa katika hospitali ya MBOZI MISHENI 

Aidha abali toka polisi zina sema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika zahanati ya kijiji cha NAMBINZO,wakati chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.

Dereva anashikiliwa na jeshi la polisi wakati taratibu za kumfikisha mahakamani zikiendelea kufuatwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa MBEYA na kamishna msaidizi DIWANI ATHUMANI ametoa wito kwa madereva kuwa makini pindi watumiapo vyombo vya moto kwa kuzingatia usalama barabarani hili kuzua ajali zinazo weza kuepukika.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment