BALAA MBEYA,UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SIRAHA (PANGA} WAZIDI KUSHAMILI.



Habari kutoka Mbeya,Airport Tankini zinasema kuwa wanyang'anyi walio pora pikipiki wamekamatwa na kukiri kuhusika katika matukio ya uporaji wa pikipiki maeneo mbalimbali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema mnamo tarehe 14.8.2013 ajira ya saa 16;50 eneo la Airport Tankini kulifanyika unyang'anyi wa pikipiki aina ya T.691 CJF aina ya KINGLION uliofanywa na watu wawili.

moja ya pikipiki 8 www.jichopembuzi@gmail.com

Aidha Diwani ameongezea kuwa aliye porwa pikipiki ni Daniel Songela mkazi wa Mbalizi alinyang'anywa na watu wa 2 waitwao Baraka Daudi,na Shadrack Essau na wote ni w
akazi wa jiji la Mbeya.

Hata hivyo sambamba na tukio hilo jumla ya pikipiki nane zinazo dhaniwa kuwa mali ya wizi zimekamatwa katika msako huko Tukuyu wilayani rungwe na watuhumiwa 6 wamekamatwa akiwemo Simon Mwanyasi,Lwitiko Hadson,Osfa  Mwamakula,Festo Gideon,Sofia Gideon,Noel Yesaya na wote ni wakazi wa Tukuyu.

Kamanda Athumani anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kupata  mali kwa njia ya mkato kwa tamaa za utajili wa haraka kwani ni kinyume cha sheria.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment