MAFURIKO DAR:WATU 13 WAPOTEZA MAISHA

Watu 13 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na mafuriko makubwa mkoani dar es salaam,Tanzania

mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sadiq meck Sadiq amesema idadi hiyo huenda ikaongezeka baada ya kupata taarifa za matukio ya mafuriko kutoka maeneo yote ya mkoa wa dar es salaam 

kwa siku tatu mfulululizo tangu ijumaa iliyopita mvua kubwa zinaendelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa vikiwemo vifo uhalibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja,hivyo kukata mawasiliano ya mikoa jirani ya pwani na morogoro na hata ndani ya mkoa wenyewe.

picha ya juu muonekano wa jiji la dar es salaam kwenye mafuriko.
karibu maeneo yote ya mkoa wa Dar es salaam yameathirika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko,huku wakazi wa maeneo ya mabondeni wakiathirika zaidi baada ya nyumba zao kujaa maji.

Mradi mwingine muhimu wa mabasi yaendayo kasi,DART unalenga kutatua tatizo la usafiri jijini Dar es salaam nao umeathiriwa na  mafuriko hayo ambapo magari,mashine na mifuko ya saruji imechukuliwa na maji na kusababisha zoezi hilo la utengenezaji wa barabara kuwa gumu.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment