Watu walionusulika wamekuwa wakieleza hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli korea kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba ,ikiegamia upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikaanza kuegamia upande mmoja anasema abilia aliyeokolewa Kim Song-Muk.
watu walikuwa wakiangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli ,lakini ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka.
bado haijafahamika kilicho sababisha kuzama kwa meli hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa hiliwabeba wanafunzi wa shule
watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa.
0 maoni:
Post a Comment