JESHI LA URUSI LA WEKWA KATIKA TAHADHARI YA MAPAMBANO.

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameviweka vikosi vyake vilioko Urusi ya kati katika "tahadhari kamili ya mapambano" na kuaamuru wanajeshi 65,000 katika eneo hilo kujihandaa kwa kufanya luteka za kijeshi za wiki moja.

waziri wa ulinzi wa urusi sergei shoigu amesema mazoezi hayo ya kijeshi ya angani na ardhini katika maeneo ya milima ya Volga na Ural yameaanza kufanyika kuanzia jumamosi juni hadi juni 28

Jumuiya ya kujihami ya NATO imesema mapema wiki hii kwamba Urusi imerudia tena kurundika wanajeshi wake kwenye mpaka wa UIkraine ambapo waasi wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipambana na vikosi vya serikali kwa wiki kadhaa katika mzozo ulioghalimu maisha ya watu 300 na kuwapoteza makazi mengine 34,000

Luteka hizo za kijeshi zinakuja siku moja baada ya Rais Petro Poroshenko wa Ukraine kutangaza  wiki moja ya usitishaji wamapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki ya nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa Amani wa vipengele vinne ambao pia unajumuisha msamaha na ahadi ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment