KLABU ya Young Africans imemshitaki mchezaji Emmanuely Okwi kwa shirikisho la soka (TFF)na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA)Kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya yanga mitaa ya twiga/jangwani mwenye kiti wa yanga bwana yusuf manji amesema wameshangazwa na kitendo hicho kilicho fanywa na viongozi wa Simba wakala wake na Mchezaji mwenyewe .
ikiwa tunasubili majibu kutoka TFF jana mchezaji huyo amesaini mkataba mwingine ,hii inaonyesha ni jinsi gani mchezaji huyo kuna watu walikuwa wakimlubuni kwa kusaini mkataba mwingine kitu ambacho amekiuka sheria za fifa za usajili
baada ya kuona jana amesajili mkataba simba ,yanga tulicho kifanya leo ni kuandika barua nyingine TFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa fidia ya Us dollar 500,000 (sawa na shilingi za kitanzania 800,000,000)kutoka kwa klabu ya Simba wakala wake na mchezaji mwenyewe.
Lengo sio kuikomoa timu ya simba bali tunacho taka ni sheria itumike ,Okwi alikuwa ameitumikia yanga kwa kipindi cha miezi sita na alibakiza mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya jangwani.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment