-Wawili wajeruhiwa
Dereva wa pikipiki aliyefahamika kwa jina moja la Temba anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 35 amenusrika kupoteza maisha akiwa na mteja wake baada ya kugongwa na gari la kampuni ya ulinzi la Security Group Africa mjini Moshi mapema leo.
Tukio hilo limetokea majira ya 2:45 asubuhi katika barabara ya Boma Road mjini Moshi likihusisha bodaboda yenye namba za usajili T 587 CYR aina ya boxer na gari lenye usajili nambari T 708 BAF aina ya Nissan.
Gari hilo la kampuni la ulinzi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Leornad Essau (34) aliyekuwa akitokea mzunguko wa Arusha kuelekea Voda House mjini humo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema gari hilo la ulinzi lilikuwa mwendo kasi mbele yake kulikuwa na bodaboda ilikyokuwa ikimwonyesha ishara ya kupinda kulia ikitokea upande wa kushoto ndipo ilipomgonga kwa nyuma na kusababisha ajali hiyo.
Mashuhuda hao waliongeza kusema madereva wa kampuni hilo wamekuwa na tabia ya kukimbiza magari yao pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo kuwahi kunywa chai na mihogo ambayo hupikwa karibu na eneo la Voda House.
“Yaani hawa madereva kila siku asubuhi wamekuwa na mashindani kama ya magari (motor rally), unafikiri wanawahi tukio fulani kumbe wala, ni kuwahi kunywa chai na mihogo hapo voda house” alisema shuhuda mmoja.
Dereva wa Bodaboda alikimbizwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi huku abiria wake mwenye jinsi ya kike (anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22 hadi 30) akikimbizwa katika hospitali ya Kilimanjaro kwa matibabu zaidi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki na Waendesha bodaboda mkoa Kilimanjaro (CWBK) Bahati Nyakiraria alisema madereva wengi hawana udereva wa kujihami kama ambavyo sheria inawaagiza kufanya hivyo.
Hata hivyo aliongeza kusema madereva wa bodaboda wamekuwa wakionewa kuwa ni wavunjaji wa sheria za usalama barabarani kumbe wakati mwingine wenye magari ndio wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuzuilika.
Maafisa wa Jeshi la Polisi walionekana katika eneo la tukio wakiendelea na utaratibu wao wa kupima chanzo cha ajali hiyo.
Posted by JAIZMELA LEO at Friday, September 19, 2014 No comments: Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
Share to Pinterest
Links to this post
Reactions:
K'NJARO UPDATE: WAANDISHI HABARI WANUSURIKA KUFA
K'NJARO UPDATE: WAANDISHI HABARI WANUSURIKA KUFA
MOSHI: JAIZMELALEO
Waandishi wa Habari watatu mkoani Kilimanjaro wanusurika kifo katika matukio mawili tofauti ya kugongana na pikipiki wakiwahi katika majukumu yao ya kazi akiwemo Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wilaya ya Hai.
Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Jumatano majira ya 4:30 adhuhuri katika eneo la Kindoroko (Double Road) mjini Moshi.
Waandishi hao wamefahamika kuwa ni Dixon Busagaga (Tanzania Daima na Clouds FM), Jackline Massawe (Radio Free Africa) na Arnold Jonathan (HabariLeo).
Arnold Jonathan anaelezea tukio hilo akiwa katika Hospitali ya St. Joseph ya mjini humo
“Asubuhi ya Jumatano, nilikuwa nikitoka nyumbani ninakoishi maeneo ya Njoro kuelekea katika kikao cha ndani chha kamati ya siasa kwenye ofisi za UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, nikiwa nimepanda bodaboda na dereva alipoigonga gari aina ya Noah iliyokuwa mbele yetu na mimi kurushwa na kuangukia juu ya gari hilo” .
Hali ya mwanahabari huyo na dereva wake inaendelea vizuri kwa sasa ingawa anadai kuwa kifua chake hakiko sawa.
Katika tukio la pili lililowahusisha wanahabari Dixon Busagaga na Jackline Massawe ambao wamelazwa katika Hospitali mbili tofauti ambazo ni KCMC na St. Joseph bado hali zao ni mbaya kutokana na majeruhi waliyoyapata.
Dixon Busagaga anaelezea tukio jinsi lilivyowakuta
“ tulikuwa tumepakiza na mwenzangu (Jackline) tukielekea Moshi Golf Club kwa ajili ya majukumu ya kikazi ndipo tulipofika katika eneo la Moshi-Arusha wakati tukilipisha gari mojawapo lililokuwa likichepuka kuelekea upande tuliopo nndipo dereva wa bodaboda alipotuvaa kwa ghafla na kujikuta tupo katika hali hii”.
Dixon ameumia katika upande wa kulia ambapo sikio lake la kulia lipo katika hali mbaya pamoja na mkono wa kushoto, wakati Jackline ameumia maeneo ya kiunoni na goti la mguu wa kulia.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki na Waendesha bodaboda mkoa Kilimanjaro (CWBK) Bahati Nyakiraria alisema madereva wengi hawana udereva wa kujihami kama ambavyo sheria inawaagiza kufanya hivyo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuwataka madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wanapokuwepo barabarani.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment