Ebola:Maafisa wa afya waliuawa

Viongozi nchini Guinea wamesema tayari wamepata maiti kadhaa za timu ya wahudumu wa afya pamoja na wanahabari waliotoweka walipokuwa wakiendeleza harakati za kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Msemaji wa serikali ya Guinea amesema kati ya miili hiyo ni ile ya wanahabari watatu wa timu hiyo.
Timu hiyo ilisemekana kupotea baada ya kushambuliwa hapo jumanne katika kijiji kimoja kilicho karibu na Mji wa Nzerekore ulio kusini mwa Guinea.
Mkurupuko wa Ugonjwa huo ndio hatari zaidi kote duniani kwa sasa, huku viongozi wakitahadharisha kwamba huenda watu zaidi ya 20,000 wakaambukizwa.
Timu hiyo ya madaktari watatu na wanahabari watu walipotea baada ya kushambuliwa kwa mawe na wakaazi wa kijiji cha Wome, walipofika katika kijiji hicho kilicho karibu na mahala ambapo mkurupuko wa Ebola ulianza.
Kwa mujibu wa mwanahabari mmoja aliyeweza kunusurika aliwaambia wanaripota kwamba alipokuwa amejificha, aliweza kusikia wakaazi hao wa Wome wakiwatafuta.
Wajumbe wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Afya walitumwa maeneo hayo lakini hawangeweza kufika kwa kutumia barabara kwani daraja lilikuwa limewekwa vizuizi.
Hapo Alhamisi msemaji wa serikali ya Guniea Albert Damantang Camara alithibitisha kwamba maiti nane zilikuwa zimepatikana na miongoni mwazo zilikuwa zile za wanahabari watatu.
Alieleza ya kwamba miili hiyo ilipatikana katika pipa moja la shule ya msingi iliyo katika kijiji hicho, na kuongeza kuwa timu hiyo iliuawa kinyama na wakaazi hao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment