Watu wapatao elfu moja kutoka jamii ya Wakurdi wa Syria wamekusanyika
kwenye eneo la mpakani wakitaka kuvuka kuingia nchini Uturuki hii leo baada
ya wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu kuviteka vijiji 21 na kuuzingira mji
wa Wakurdi kaskakazini mwa Syria. Taarifa zinasema watu hao ambao wengi
ni wanawake na watoto wamekusanyika kando ya ua wa seng'enge katika
mpaka wa kuingia Uturuki kwenye kijiji cha Dikmetasa uliko kilomita 20 kutoka
mji wa kikurdi wa Ayn Al-Arab nchini Syria ambao pia unafahamika kama
Kobani kwa lugha ya Kikurdi. Mashambulizi dhidi ya mji huo wa Kobani
yamechochea wanamgambo wa Kikurdi kuwatolea mwito vijana kutoka eneo
la kusini mashariki ya Uturuki ambalo linakaliwa zaidi na Wakurdi kujiunga
katika mapambano hayo dhidi ya waasi wa Dola la Kiislamu. Mwito huo
umekuja siku chache tu baada ya jeshi la Marekani kusema msaada wa
Wakurdi wa Syria utahitajika katika mapambano dhidi ya waasi hao wa itikadi
kali.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment