Aliyelala hapo siyo mbwa, ni gari ambalo limebadilishwa na kuwa na umbile la mbwa.
Kweli majuu hamnazo! Mkulima mmoja wa mjini Sussex amelibadili gari lake aina ya Peugeot lionekane kama mbwa na akasema bado anafikiria nini cha kufanya.
Dave Isaac (46), alitumia Paundi 2,000 (takriban Shs. 4.8 milioni) kuipamba gari hiyo ya familia kwa manyoya na kulifanya lionekane kama mbwa wake kipenzi aliyekufa.
Likiwa na mwendokasi wa juu wa maili 40 kwa saa, mkulima alilichukua gari hilo lenye muonekano wa mbwa na kwenda nalo kwenye shamba lake lenye ukubwa wa ekari 180, jirani na Battle, East Sussex huku akiwaacha wengi wakiwa na mshangao.
"Najua ulikuwa ni uendawazimu kufanya hivi lakini nilikuwa namuenzi mbwa wangu Floss aliyekufa," alisema.
"Kwa hiyo mimi na rafiki yangu tukatengeneza 'bodi' la gari lionekane kama umbile la Floss wakati tukiwa kwenye banda langu, nikiiga walau kila kitu kama mbwa wangu alivyokuwa anaonekana.
"Mbwa wangu alikuwa na manyoya kama kondoo, na kondoo hawafahamiki kutokana na uelewa wao na haikuwa rahisi kugundua tofauti lakini tulifurahi sana."
Tatizo likaibuka namna ya kuliingiza gari hilo barabarani, ambalo halijasajiliwa kupita kwenye barabara za umma, hadi zile za kwenda mashambani mpaka kwenye mageti ya shamba lake.
Na gari hilo, ambalo lilihitaji mbao za pembeni ili kuziunganisha kwenye chassis na kubandika manyoya, lilikuwa linachukua nafasi kubwa kwenye banda la shamba hilo ambalo lina pilika nyingi.
Akaongeza: "Haya yalikuwa mambo ambayo hatukuyafikiria kabisa wakati tulipokuwa tunatengeneza 'bodi' sasa kwa moyo mkunjufu naliingiza sokoni kupitia E-bay."
Bwana Isaac anatumaini kwamba gari hilo maarufu kama 'Floss the sheep dog' linaweza kuwavutia waandaaji wa matamasha ama wahisani wa masuala ya mbwa: "Kama litachukuliwa katika mikono salama nitakuwa na furaha," alisema.
0 maoni:
Post a Comment