Viongozi waaswa kutotumia uongozi wa serikali za mitaa kupitisha wagombea wao



Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Iramba wakati wa ziara ya kuimarisha chama



Wakazi wa kijiji cha Kiliminzowho wakisubiri matokeo baada ya kupiga kura za maoni



Wakazi wa Kijiji cha Iramba wakifatilia mkutano kwa makini


Na Mathia Canal, Mufindi
Viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wameaswa kutotumia nafasi ya kura za maoni kupitisha wagombea wanaowataka badala yake kupitisha wagombea wanaopendwa na kupigiwa kura nyingi na wananchi.

Hayo yamesemwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Iramba na Ikimilinzowho Kata ya Itandula wakati wa ziara yake ya kuimarisha chama Wilayani humo.

Mtaturu alitoa rai hiyo kwa viongozi wa chama hicho ngazi ya Shina, tawi na Kata huku akisema kuwa kwa yeyote atakaye pitisha majina ya watu ambao hawajachaguliwa na kukubalika na wananchi itakuwa ndio tiketi yao ya kuvuliwa uanachama ili kulinda heshima ya chama hicho ambayo bado haijavunjika tangu kuanzishwa kwake.

"Leo ninawataka viongozi kutotumia nafasi hii ya kura za maoni kama njia ya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Ubunge na udiwani utakaofanyika mwakani, endapo kama atajitokeza kiongozi wa aina hiyo sisi kama chama cha mapinduzi hatutamvumilia hata kidogo" Alisema Mtaturu

Alisema kuwa kila unapokaribia wakati wa uchaguzi kila chama kina utaratibu wake wa kupata mgombea, hivyo kwa upande wa CCM kila mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kutokana na ngazi anayogombea kama amejipima na kuona kuwa anastahili.

Katika ziara yake katika Kijiji cha Iramba na Ikimilinzowho, Mtaturu aliamua kusimamia uchaguzi wa kupitisha mgombea anayekubalika baada ya viongozi wa chama hicho kijijini hapo kushindwa kupata wagombea kutokana na dhamira ya kutaka wagombea wao wapite badala ya kupitisha wale wanaopendwa na wananchi.

Sambamba na hayo alitimiza ahadi aliyoitoa wakati wa ziara yake miezi miwili iliyopita kwa wananchi hao ya kuchangia mifuko 10 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Ikimilinzowho.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kijiji hicho Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, France Nkanu alimpongeza katibu huyo kwa kuchangia mifuko ya saruji huku akitumia nafasi hiyo pia kumshukuru Mericelina Mkini ambaye ni MNEC Wilaya ya Mufindi kwa kuchangia mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi huo wa Zahanati.

Akizungumzia swala la katiba pendekezwa Mtataru aliwaomba wananchi hao kuipigia kura ya ndio kwani katiba hiyo ina maslahi mapana kwa Taifa na sio kejeli za vyama vya upinzani ambavyo vinajipanga kupinga kwa maslahi yao binafsi na sio wananchi.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment