MBUNGE VITI MAALUMU NJOMBE AUNGANA NA WANANCHU KUZIBA SHIMO KUBWA LILIZO FUNGA BARABARA

WATUMIAJI wa barabara ya nyuma ya
uwanja wa ndege wameamua kujitolea kuziba shimo lililokuwepo katika barabara
hiyo ambalo lilikuwa likileta ushumbufu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wamesema kuwa wamekunbwa na adha ya kupita katika eneo hilo  kwa muda mrefu hivyo wameamua kujitoa kufanya
ukarati wa eneo hilo korofi.
Wamesema kuwa eneo hilo lilikuwa
kama limesahaulika na wahusika na kuwa kwa sasa watapita bira kunasa kwa magari
na pikipiki zao.
Mmoja wa wananchi hao Emmanuel
Mapunda alisema kuwa serikali kuna uzembe iliufanya katika eneo hilo ambalo
kulitakiwa kuwekwa kalavati ambalo lingetoa maji kutoka upande mmoja kwenda
upade unao fuata.
Alisema kuwa chanzo ya kuharibika
kwa barabara hiyo kuwa ni kuwapo kwa maji kujaa kwenyekona na kushindwa sehemu
ya kwenda mvua zikinyesha.
Hata hivyo dereva wa bodaboda Lemigiusi
Mtewele alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa nio kero kubwa kwao kwa kuwa ilikuwa
ni sumbufu na kuwa sehemu hiyo imekuwa ikiharibika mara kwa mara kipindi cha
mvua.
Alisema kuwa yeye amesha wahi
dondoga katika eneo hilo akiwa amebeba mzigo huku wakilazimika kupita katika
maeneo ambayo sio barabara.
Mbunge wa viti maalumu mkoa w
anjombe Licia Mlowe anaamua kuungana na wananchi hao kuhakikisha kuwa eneo hilo
linapitiba na kuhakikisha kuwa mvua zinazo endelea kunyesha haziikati tena
barabara hiyo.
“Eneo hilo lilikuwa ni kelo kwa
wananchi na tumekungana na wananchi wanaotumia barabara hii na kuanza kuchimba
ili kuweba bomba ambalo litakuwa likihamisha maji yaliyo kuwa yakijaa katika
kona ya barabara na kusababisha uharibifu,” alisema Mlowe.

Barabara
hiyo inaingia katika mitaa ya Nzengelendete nyuma na uwanja wa ndege na kipindi
baraabara hiyo imeziba wananchi walilazimika katikati ya uwanja wa ndege
kupukana na adha hiyo.

from Blogger http://ift.tt/1Lu2FHL
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment