DIWANI wa kata ya Lupombe amezuia uhamisho wa mtendaji wa kijiji cha Luponde Wilayani Njombe Stiniususi Mlowe anaye daiwa kukuhusuka na upotevu wa fedha za vocha za Ruzuku za pembejeo za zaidi ya milioni tatu mpaka atakapo zilejeha.
Fedha hizo zinadaiwa kuwa ni za vocha 40 za ruzuku ya pembejeo za kilimo katika vijiji vya Luponde na Lusitu ambapo vicha hizo zilitakiwa kupatiwa wananchina kaya masikini.
Akizungumza na wananchi diwani wa kata ya Luponde Ulrick Msemwa alisema kufuatia matumizi mabaya ya vocha za pembejeo za kilimo yaliofanywa na mtendaji huyo, afisa utumishi wa halmashauri ya mji wa Njombe hatakiwi kumuhamisha hadi atakapo maliza malipo ya fedha shilingi milioni mbili na laki nne za kijiji cha Luponde na shilingi laki 8 za kijiji cha Lusitu sawa na shilingi milioni tatu na laki mbili.
Katika kikao hicho wazazi wa mtendaji huyo baada ya kukili kuwapo kwa ubadhirifu huo wazazi wake wameamua kulipa fedha hizo ndani ya siku 30.
“Vocha hizo zitalipwa ndani ya siku 30 na fedha hizo zitalipwa na wazazi wa afisa mtendaji, na baada ya hapo fedha zizo zitafanya kazi zingine baada ya kurejeshwa na wazazi tuwe tunawauliza watoto wetu amefanya kazi mda mfupi anamali zinazo zidi mshahara tuwaulezi wasio endelea tusiwashangae,” alisema Msemwa
Hata hivyo licha ya vocha hizo kutakiwa kutumika kwaajili ya wananchi na kaya zilizo na uwezo duni kwaajili ya kulipa pembejeo za kilimo lakini wanadaiwa kupewa watu wenye uwezo na watumishi wa umma.
Mtendaji huyo alisema kuwa vocha hizo alizigawa kwa mratibu elimu kata, afisa mifungo, mwalimu mkuu wa sule ya Luponde, afisa afya, na kuna baadhi ya watu wa chama cha mapinduzi kupatiwa, na kuwa yeye mwenyewe alijigawia.
Wakizungumza kwenye kikao kifupi katika ofisi ya serikali ya kijiji cha Luponde baadhi ya wananchi na wajumbe wa serikali ya kijiji hicho wamesema kutokana na wazazi wa afisa mtendaji wa kijiji hicho kukili kulipa fedha hizo ndani ya siku 30 baada ya kujiridhisha kuwa mtendaji huyo anamakosa wanaomba Halmashauri kutohamishia sehemu nyingine kuendeleze tabia hizo wanaobainika na tuhuma za ubadhirifu.
Hata hivyo halmashauri tayari imetoa uhamisho kwa mtendaji huyo licha ya kutuhumiwa kuhusika na wizi huo amekili kupewa barua ya uhamisho na afisa utumishi wa halmashauri ya mji wa Njombe kuhamia kijiji cha Uliwa na wa Uliwa kuhamia kijiji cha Luponde uhamisho wa kawaida si kwa vile ametuhumiwa.
from Blogger http://ift.tt/22lDsck
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment