Akiwa ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa zuio hilo linawahusu wa wafanyabiashara wanaotumia magari yenye uzito usio zidi tani 30 ambapo ndani ya miezi hiyo watakata vibari vya kupitisha uzito huo na baada ya hapo hakuta kuwa na vibali vya kupitisha uzito huo.
Alisema kuwa wafanya bishara hao watapitisha mizingo yenyeuzito wa kuanzia tani 30 kushuka chini kwa kukata vibari ofisi za wakala wa barabara tanzania mkoa wa njombe Tanroads na baada ya miezi hiyo miwili hakuta ruhusiwa uzitu unaozidi tani 10.
Alizitaja barabara zinazo husika na zuiohilo baada ya miezi miwili kuwa ni pamoja na barabara ya Kibena mpaka Lupembe kuunganisha na Morogoro, barabara ya Rambazani njombe mjini mpaka wilayani makete na barabara ya Itoni njombe mjini mpaka wilayani Ludewa ambazo zimeingizwa katika mpango wa kukarabatiwa kwa kiwango cha lami.
hata hivyo mkuu wa mkoa aliongeza kuwa kuwepo kwa zuio hilo kutazinusuru barabara hizo na uharibishi na kurahisisha upitishaji wa huduma ya usafiri bila kadhia na kusema vibari hivyo vitatolewa kwa kuchangiwa kiasi cha dola za kumalekani 20 kwa kibali.
Walengwa wa agizo hili ambao kwa sehemu kubwa ni wasafirishaji wa mazao kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wakiwemo madalali wamepokea kwa hisia tofauti agizo kwa kuhofia mtikisiko wa uchumi
Wamesema agizO hilo litaathiri kwa sehemu kubwa uchumi wa wakulima kwa kuwa mazao yatashuka bei huku wakishauri serikali kuacha mpango wake huo katika kipindi hiki cha mavuno ya viazi na kusema kuwa mzingo wa gharama utamuangukia mkulima.
Wiibart Mchaga ni Miongoni wafanyabiashara wanao gushwa moja kwa moja na mpango huo wamesema kuwa wataangalia kama biashara itawakata basi wataachana nayo na kutafuta biashara nyingine.
Alisema kuwa wafanyabiashara kwa kuwa ndio wenye pesa basi wataangalia kuhusiana na soko kama lina lipa basi kuendelea lakini mzigo wa kufaulisha watawaachia wakulima.
Pamoja mawazo mazuri ya serikali wadau wa usafirishaji wakiwemo madalali na wakulima hawajashirikishwa kutoa maoni yao na wangetakiwa kujiandaa kuepuka madhara ya kudorola kwa uchumi
from Blogger http://ift.tt/253Xfiw
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment