KESI YA KUPINFGA MATOKEO YA JIMBO LA NJOMBE KUENDELEA MACHI 9

MAHAKAMA  Kuu Kanda ya
Iringa imetoa uamzi wa kufanyiwa marekebisho mapungufu yaliyowekewa pingamizi
na Wakili wa serikali Apimaki Mabrouk dhidi ya mlalamikaji Emmanuel Masonga
katika kesi ya uchaguzi inayowakabili Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Edward Mwalongo,
Msimamizi wa Uchaguzi wa wa jimbo hilo Eliminata Mwenda na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Akitoa uamzi huo katika ukumbi wa mahakama hiyo mjini Njombe,
Jaji Jacob Mwambegele, amesema pamoja na kukubaliana pingamizi liliowekwa na
wakili wa serikali Mabrouk kwamba katika ombi la kesi hiyo aya 7,8,9 na 10
zinamapungufu kisheria kutokana na maelezo yake kutojitosheleza, lakini
hakubaliani na ombi lake la kutaka kuzifuta ili shauri hilo liondolewe
mahakamani.
Badala ya kuzifuta aya hizo Jaji Mwambegele, ametoa siku saba  kwa mlalamikaji katika kesi hiyo Masonga,
ambaye alikuwa mgombea wa ubunge wa Chadema katika jimbo hilo kufanyia
marekebisho, na kwamba akishindwa ndani ya muda huo, kesi hiyo itafutwa na
atatakiwa kulipa gharama zote.
Awali Machi mosi, mwaka huu Wakili wa serikali Apimaki
Mabrouk aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hati ya shauri ya kesi hiyo kwa kile
alichodai kuwa hoja za mlalamikaji katika hati yake ya maombi katika aya 7, 8, 9
na 10, zina maelezo yasiyojitosheleza hivyo itakuwa ngumu kwa upande wa
walalamikiwa kujitetea, na kwamba hatua hiyo itasababisha kesi hiyo kuchukua muda
mrefu hadi kutolewa uamzi.
Mara baada ya uamzi huo nje ya Ukumbi wa mahakama Wakali wa
Masonga, Edwin Swale amesema watafanya marekebisho ndani ya muda uliotolewa na mahakama
ili kesi iweze kuendelea machi 16 mwaka huu.

from Blogger http://ift.tt/1RzOQd3
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment