Wanne wafa ajari ya daladala,Fuso Dar



WATU wanne wamethibitishwa kufa baada ya kutokea ajali mbaya maeneo ya Al hamza jirani na daraja la Tabata Matumbi.
Miongoni mwa  waliokufa ni Godfrey Nyawenga na wengine watatu bado kutambuliwa.
Aidha majeruhi  25 akiwamo mtoto wa mwaka mmoja walipatikana na watu watano wako katika hali mbaya na wamekimbizwa Muhimbili kutoka hospitali ya amana akiwamo mtoto wa mwaka mmoja.
 
ng’ombe wakiwa wametawanyika



Lori lililobeba ng’ombe




Ajali hiyo mbaya  kabisa ilihusisha magari matatu likiwemo Dalalada ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo,  lori la mchanga na lori la ng’ombe. 
Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limebeba ng’ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

from Blogger http://ift.tt/1UeqJp1
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment