Kesi ya kupinga matokeo yaendelea Njombe

Kuanzania Kushoto aliye ni kuwa mgombea Emanuel Masonga na wa pili mbunge Edwadi Mwalongo wakiwa mahakamani katika mahakama kuu ya Iringa inayo fanyia vikao vyake mkoani Njombe
KESIya uchaguzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyo mtangaza mbunge wa Njombe kusini Edward Mwalongo inaanza kusikilizwa Machi 18 mwaka huu baada ya kupita hatua ya mapingamizi huku mashahidi wakijulikana siku hiyo.
Kesi hiyo namba 6/2015 katika mahakama kuu kanda ya Iringa iliyofunguliwa na aliye kuwa mgombe wa Chadema jimbo la Njombe Emmanuel Masonga ambapo anawashitaki Mbunge Mwalongo, msimamizi wa uchaguzi mkurugenzi wa mji Njombe Eluminata Mwenda na manasheria wa serikali jana ilikuja kwaajili ya kupeleka mashahidi kwa upande walalamikaji.
Akizungumza mahakamani hapo mbele ya jaji Jacob Mwambegele wakili wa masonga Edwin Swale alisema kuwa kesi tayari mashahidi wao wamesha waandaa kama mahakama ilivyo wataka kuwasilisha mashahidi ndani ya siku saba.
Swale aliiambia mahakama kuwa Machi 14 ambapo zilikuwa zinakoma siku saba walizo pewa walipeleka ushahidi  wao na ikiwa tayali kwa kuanza kutoa ushahidi wao.
Jaji Mwambegele alisema kuwa tayari ushahidi huo wameupokea na kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maandalizi ya awali Machi 18 mwaka huu na kuwataka mawakili wa pande zote mbili kukaa pamoja ili kuangalia vitu vinavyoleta utata vinachunguzwa na kuviweka sawa ili itakapo anza isichukue mda mrefu.
“Nitoe tu angalizo kwa mawakili wote make pamoja na muangalie kesi yenu itakaaje na ili kusije kukatokea mkanganyiko siku hiyo na kusababisha kesi kuchukua mda mrefu kaeni mjadili vikwazo mviondoe mapema mkishauriana,” alisema Jaji Mwambegele.
Akizungumza na wananchi walip fika mahakamani hapo nje ya ukumi wa mahakama Wakili Swale alisema kuwa kesi hiyo inaanza kusikilizwa kwa hatua ya maandalizi na kuwa kulitokea mkanganyiko baada ya kuwekewa pinga mizi kutokana na mashahidi walio nao katika kesi hiyo.
Alisema kuwa “Tulipo ingia kwa jaji mawakili wa upande wa washitakiwa walikuwa wakipinga uwingi wa mashahidi tulionao lakini tumemaliza utata na wananchi jitokezeni katika kila hatua kushuhudia,” alisema Swale.

from Blogger http://ift.tt/22lDukh
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment