Madiwani waanza semina ya siku 4 kwaajili ya kuelimishwa Njombe

 Baadhi ya madiwani na watendaji wa halimashauri za Makete na wanging’ombe wafuatilia jambo katika semina kwao inayo tolewa katika Mradi wa PS3
 Kiongozi wa mradiwa wa PS3 akizungumza wakatiwa kumkaribisha mgeni tasimi katika semiana kwa madiwani na watendaji ya kuwa weka imara katika mifumo yao ya uterndaji na utoaji huduma kwa jamii.
 Mgeni rasimi na kaimu mkuu wa mkoa wa njombe na mkuu wa wilaya ya Makeye Daud Yasini akifungua mkutano wa semiana kwa Madiwani ya siku 4 mkoani Njombe 
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpta Mshama akizungumza na madiwani wa kata za Makete na Wangingombe.

IMEDAIWA kuwa bila kuwapo kwa ushirikiano mzuri baina ya
wananchi na serikali kufuatia kutambiliwa kwa kuwepo kwa ushirikiano huo
halmashauri za Wangingombe na Makete zimeanza kupatiwa elimu kwa madiwani wake
ambao ni wawakilishi mukumu wa wananchi.
Akifungua semina ya siku nne kwa madiwani, watendaji na
wenyeviti wa halmashauri za Makete na Wanging’ombe, yanayo tolewa chini ya
mradi wa uboreshaji ya huduma kwa umma kwa serikali za mitaa wa Public Sector
system Strengths (PS3) kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe na mkuu wa wilaya ya Makete
Daudi Yasini.
Yasini alisema kuwa serikali haita weza kufanya shughuli za
maendeleo kama kutakuwa na mpasuko wa kiutendaji ma maelewano baina ya Madiwani
na watendaji wa halmashauri.
Alisema kuwa madiwani ni kiunga muhimu baina ya serikali na
watendaji wa serikali madiwani waasipo kuwa vizuri katika utendaji wao
watasabaisha shughuli za maendeleo kuwa ni ngumu kutekelezwa na serikali katika
kata zao.
Alisema kupitia elimu hiyo serikali itaenda kufanya shughuli
zake bila kuwapo kwa vikwazo kwa kuwa madiwani na watendaji wote watafanya kazi
kwa mipaka yao ya kiutendaji.
Aidha kwa niaba ya watendaji na madiwani akitoa shukrani
baada ya kufunguliwa kwa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpta
Mshama alisema kuwa serikali inatoa elimu hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa maendeleo
yanaonekana.
Alisema kuwa kupitia elimu hiyo madiwani hawata kuwa na tabia
ya kuazimia wetendaji kuondolewa nyazifa za watendaji na baada ya elimu
kutawasaidha kufanyakazi kila mtu kwa nafasi yake.
Aidha Kiongozi wa mradi huo wa PS3 Peter Kilima, alisema
kuwa ni kutokana na nafasi kubwa waliyonayo ya kuwasirisha matatizo ya wananchi
shirika la USAID limeonelea Kutoa mafunzo hayo kwa madiwani.

from Blogger http://ift.tt/1UuDqIB
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment