MAKETE,WANGING’OMBE ZACHAGULIWA MAFUNZO AWAMU YA KWANZA UIMARISHAJI MIFUMO SEKTA ZA UMMA


Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Njombe Richard Moshi(kulia) akimshukuru Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima mara baada kufunga mafunzo ya uzinduzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa Halmashauri za Mkoa wa Njombe.



Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt.Peter Kilima akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za umma



Mwezeshaji kutoka mradi wa Mifumo ya Uimarishaji Sekta za Umma Bunto Mbozi akiwasilisha mada kwenye kikao kilichowahusisha Wakurugenzi, wakuu wa idara, wenyeviti na viongozi wa halmashauri 6 za mkoa wa Njombe



Kiongozi wa uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Dkt. Peter Kilima akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe Richard Moshi taarifa ya uteuzi wa Halmashauri mbili za Makete na Wanging’ombe kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya awamu ya kwanza kwa Madiwani wa Halmashauri hizo.



Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Richard Moshi akitanganza Halmashauri mbili za mwanzo zilizochaguliwa kushiriki mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa madiwani.



Mkurugenzi Msaidizi, Uismamizi Rasilimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mmbaga akitoa nasaha mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma mjini Njombe.



Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma wakiwa kwenye kazi za vikundi



Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari 



Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Miriam Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo kwa watendaji an watumishi wa idara halmashauri za wilaya mkoa wa Njombe.



Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpter Mshama akizungumza kwenye kikao kilichozishirikisha Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe



Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akihakiki taarifa zake kabla ya kutangazwa kwa Halmashauri mbili za Makete na Wanging’ombe kushiriki mafunzo kwa madiwani juu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma.



HALMASHAURI 2 za Makete na Wanging’ombe mkoani Njombe zimechaguliwa kuingia katika awamu ya kwanza ya mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la Msaada la Kimataifa la Marekani USAID yatawahusisha Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi pamoja na wakuu wa Wilaya.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa Halmashauri hizo Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima alisema Halmashauri hizo zimechaguliwa kuwa za mwanzo kushiriki mafunzo hayo kutokana na changamoto walizonazo.
‘’Vigezo vya uhitaji vimewapa nafasi ya kwanza kushiriki mafunzo haya kwa Madiwani ingawa halmashauri zote za Mkoa wa Njombe zitapata mafunzo hayo kwa awamu ya pili’’
Alisema mafunzo hayo yanatarajia kuanza Jumatatu ijayo mjini Njombe na kutolewa na wataalamu wa mafunzo kutokea mjini Dodoma.
Akizungumzia kuteuliwa kwa Halmashauri ya Makete,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Egnato Mtawa alisema anaamini changamoto zilizopo zimetoa kipaumbele kwao kuwa wa mwanzo kupata mafunzo hayo.
‘’Changamoto za Wilaya yetu zimetupa kipaumbele kuteuliwa wa mwanzo kupata mafunzo kwa Madiwani,tuna changamoto za jiografia na Miundo mbinu, tunaamini hatimaye changamoto tulizonazo zitapatiwa ufumbuzi’’ alisema Mtawa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpter Mshama alisema mafunzo hayo kwa Madiwani yataongeza weledi wa utendaji kazi kwa watumishi kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mpya.
Awali akizungumza mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi, Usimamizi wa Rasilimali watu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Miriam Mmbaga alisema kukosekana kwa maadili kwa watumishi wa umma ndiko kunakosababisha Halmashauri nyingi zipate hati zenye mashaka.
Alifafanua kuwa maadili yanayoelezwa ni yale yale yaliyopo katika imani za dini kwa kuwa vitabu vya dini zote zinapinga vitendo viovu ikiwemo rushwa.
‘’Dini zote zinapinga rushwa, maadili ya utumishi wa umma ni yale yale yaliyopo kwenye vitabu vya Uislamu na Ukristo,’’ alisisitiza.

from Blogger http://ift.tt/1RQ6k4b
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment