Utafiti: Misitu na mazingira vikisimamiwa ipasavyo vitaboresha maisha ya wananchi


Dr. Nicole Cross-Camp ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha East Anglia cha nchini Uingereza chini ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation) akitoa mada kuhusiana na matokeo ya utafiti kuhusu changamoto wanazozipata wanakijiji katika utunzaji wa misitu kwa wadau kutoka Wizara mbalimbali pamoja na Sekta binafsi.
Maneja Mradi, Lasima Nzao akiwasilisha matokeo ya utafiti uliopo chini ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation). Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Mistu na Mazingira kutoka Serikalini, Taasisi na Mashirika binafsi walikutana na watafiti hao ili kujadili matokeo hayo ya utafiti na kuweza kuchanganua mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto na faida zinazotokana na usimamizi wa misitu kwa wanajamii wanazozungukwa na hifadi ya misitu hapa Tanzania.

Akizungumza na Lasima Nzao na Dr Nicole Gross-Camp walisema kuwa utafiti huo uliofanyika katika vijiji nane vya wilaya mbili, halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini na wilaya ya Kilwa kuanzia Septemba 2014 na kumalizika september 2016 na ulikuwa “unaangalia mchango wa misitu inayosimamiwa na Jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maisha kwa wanakijiji husika”. 

Utafiti unaonyesha  kuwa mistu na mazingira ikisimamiwa  ipasavyo inaweza kuboresha maisha ya wananchi walio vijijini kwa kuwa wanajamii wanapenda mfumo wa misitu ya jamii japokua bado kuna changamoto nyingi katika usimamizi wa misitu kwa wanajamii hasa misitu inayosimamiwa na Jamii.

Utafiti huo ulidhaminiwa na ESPA, UKAID, NERC na ESRC na ulifanywa na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha East Anglia UEA nchini Uingereza Dr Nicole Gross-Camp akishirikiana na mtafiti kijana wa kitanzania, Lasima Nzao ambaye pia alikua meneja wa mradi wa Utafiti huo.
Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akichangia mada baada ya wataalamu kuwasilisha utafiti uliofanyika katika vijiji nane ndani ya wilaya mbili.
Mshauri wa masuala ya Misitu na Mabadiliko ya Tabianchi, Faustine Ninga akichangia mada kuhusu  utafiti uliofanyika katika wilaya mbili kuhusu mchango wa jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maishaya wanajamii.
 Gabriel Marite Ole Tuke
Msimamizi wa Maliasili kutoka Mkoani Dodoma, Sanford Kway akichangia mada
Picha ya pamoja

from Blogger http://ift.tt/2cqZBkB
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment