WALIMU WAO CHAPA WANAFUNZI MKOA WA MBEYA WATAFUTWA.








Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania Mwigulu Nchemba amewaagiza maafisa wa serikali kuwasaka walimu watatu wa mafunzo ambao wanadaiwa kumpiga mwanafunzi shuleni.
Video ambayo inadai kuonyesha tukio la mwanafunzi huyo akipigwa imesambaa sana mtandaoni Tanzania na Kenya.
Kupitia taarifa, Bw Nchemba, amesema uchunguzi wa awali unaonesha tukio hilo lilitokea katika shule ya upili ya Mbeya tarehe 28 Septemba.
Walimu hao walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo.
Anasema mwalimu mmoja alikuwa amewapa wanafunzi zoezi la Kingereza lakini baadhi ya wanafunzi wakasusia kulifanya na ndipo mwalimu mmoja "alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo."
"Ndio (hapo) walimu wakamchukua na kumpeleka staff room (chumba cha walimu) na kuanza kumpiga vile," amesema Bw Nchemba.
Tangu kutokea kwa kisa hicho, inaarifiwa mwanafunzi huyo hajaonekana shuleni tena.
Image copyright Other
Image caption Video ya kisa hicho imesambazwa sana mtandaoni Kenya na Tanzania
Walimu wote wanaodaiwa kuhusika katika kumpiga mwanafunzi huyo hawapo shuleni Mbeya kwani wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao.
"Polisi wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali," amesema Bw Nchemba.
"Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo."
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment