MCHEZAJI ALIYE INGIA MSALANI NA MWANAMKE AADHIBIWA.






Mchezaji wa timu ya raga ya New Zealand Aaron Smith amepigwa marufuku kucheza mchezo mmoja baada yake kuingia msalani na mwanamke katika uwanja wa ndege mjini Christchurch.
Hilo ni kinyume na kanuni za timu hiyo ya taifa.
Atakosa mchezo wa Ubingwa wa Raga dhidi ya Afrika Kusini mjini Durban.
Kocha mkuu wa All Blacks Steve Hansen amesema Smith mwenyewe amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Hansen ameongeza kwamba mchezaji huyo wa miaka 27 anahisi kwamba amevunja moyo timu yake, familia yake na mpenzi wake.
"Ameomba kwenda nyumbani kushughulikia masuala ya kibinafsi ambayo yameibuka kutokana na kisa hicho na tuna furaha kumsaidia katika hilo," amesema Hansen.
Kocha huyo amesema adhabu hiyo iliafikiwa na kundi la viongozi wa timu ambalo lilijumuisha wachezaji.
Smith amechezea New Zealand mashindano 54 tangu aanze kuwachezea mwaka 2012.
Baadaye mwaka 2012, alizuiwa kucheza kwa muda kwa kuvunja amri ya kutotoka nje.
Mwaka 2014 alitua picha yake ya utupu kwenye Snapchat ambayo ilisambazwa sana mitandaoni.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment