BARCELONA WAPIGWA 4G, MASHABIKI WA ARSENAL WAUZA TIKETI ZAO ZA MCHEZO WA MARUDIANO

Katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya uliopigwa jana, timu ya Barcelona ambayo inasifika kuzifanyia ubabe timu inazokutana nazo iligeuzwa kuwa nyanya na wenyeji wao wa jijini Paris, Ufaransa, klabu ya PSG.
Barcelona walidhalilishwa katika mchezo huo kutokana na magoli mawili yaliyotiwa kimiani na mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Man United – Angel di Maria pamoja na magoli kutoka kwa Julian Draxler na Edinson Cavani katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo katika hatua ya 16 Bora ya Klabu Bingwa Ulaya ulioisha kwa Barcelona kupokea kichapo cha goli 4.
Mchezaji Angel di Maria alikuwa katika kiwango cha hali ya juu kabisa katika kumiliki mpira na kuwasumbua walinzi wa Barca. Mpira wa adhabu alioupiga moja kwa moja kambani pamoja na goli lake la pili alilofunga akitumia uwezo binafsi vilitosha kumfanya awe mchezaji bora wa mechi hiyo, ‘man of the match.’
Miamba hiyo ya Katalunya sasa ni kama imechungulia kaburi na inaweza kuwatia doa kampeni yao ya kubeba makombe matatu msimu huu kwakuwa ina kibarua kikubwa cha kuhakikisha wananshinda goli 5-0 ili kuwawezesha kucheza robo fainali ya mashindano hayo bila kutegemea dakika za nyongeza wala mikwaju ya penati.
Wachezaji wa PSG wakishangilia baada ya mechi ya jana
Kwa upande wa pili, Meneja wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger anahitajika kufanya maajabu kuhakikisha timu yake inasonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya jana kupokea kichapo cha mbwa mwizi walipokaribishwa jijini Munich na wenyeji wao Bayern Munchen.
Katika mchezo huo wa raundi ya kwanza kuzikutanisha timu hizo katika hatua ya 16 bora, Arsenal alipokea kipigo cha goli 5 kwa 1 na kufanya hali kuwa mbaya sana kwao katika mchezo wa marudiano utakaopigwa tarehe 7 mwezi Machi pamoja na mechi hiyo kuchezwa katika uwanja wao wa Emirates jambo linaloonekana limewakatisha tamaa hata mashabiki wanazi wa Arsenal.
Kufikia saa 3.40 usiku, mchezo huo ulipokuwa unakaribia kuisha, tovuti ya timu hiyo ilionesha kuwa uwanja huo wenye viti 60,000 ulikuwa una rangi nyekundu tupu – ikimaanisha tiketi kwa ajili ya kuangalia mchezo wa marudiano kati ya timu hizo zilikuwa zimeshanunuliwa zote.
Dakika 18 baadaye, nafasi zilianza kuonekana kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi zao kuanza kuziachia.
Saa 4.12 usiku, siti za nyuma ya goli ambalo wapenzi wengi wa Arsenal hupenda kukaa zilionekana kuwa wazi, na ilipofikia saa 4.42 usiku karibia kila jukwaa lilionekana kuwa na siti nyingi zilizo wazi.

from Blogger http://ift.tt/2lbkINC
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment