HAKIMU NA KARANI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA RUSHWA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mara imewapandisha kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma, Swalala Mathayo (40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Marshal Mseja, alidai watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000.
Alidai Hakimu Mathayo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa,wakati karani Masatu anatuhumiwa kushiriki katika kuiomba rushwa hiyo.
Mseja alidai chanzo cha madai hayo ya rushwa ni kuwa hakimu huyo alitoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili kwa Magdalena Aloyce (29) mkazi wa mtaa wa Makongora mjini Musoma.
Alidai kwa vile mtuhumiwa alifungwa akiwa na mtoto mdogo wa miezi 10 na kuwaacha wengine wawli bila uangalizi, ndugu zake walimfuata mkuu wa gereza na kuomba mfungwa huyo apewa kifungo cha nje aweze kuhudumia familiya yake ambayo inamtegemea.
Ndugu walipewa maelekezo na mkuu wa magereza kwenda kwa ofisa wa ustawi wa jamii na walipofika walihudumiwa na kujaziwa fomu namba 12 kwa mujibu wa Sheria ya Kutumikia Jamii, alisema.
Alisema fomu hiyo ilitakiwa kuidhinishwa na hakimu aliyetoa hukumu hiyo.
Mseja alidai hakimu huyo hakuweza kufanya hivyo bali alitengeneza mianya ya kudai rushwa kwa kumuhusisha karani wake na hapo ndipo ndugu hao walipotoa taarifa Takukuru na kuwekwa mtego na hatimaye kukamatwa na rushwa hiyo ya Sh 200,000.
Watuhumiwa hao walikana mashitaka na wapo nje kwa dhamana hadi Machi 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Na Shomari Binda-Mtanzania Mara

from Blogger http://ift.tt/2kSOybi
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment